Ticker

6/recent/ticker-posts

Raheem Sterling kutua Chelsea kwa £50m

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  • Raheem Sterling anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Chelsea kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 50.Raheem Sterling anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Chelsea kabla ya kununuliwa kwa dau la pauni milioni 50 akitokea Manchester City.

Sterling anaondoka Etihad kufuatia miaka saba yenye mafanikio makubwa ambapo ameisaidia City kushinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza hapo awali alikuwa akihusishwa kuhamia Barcelona lakini Chelsea wamefanya jitihada kubwa kuhakikisha wanamsajili katika msimu huu wa majira ya joto.

Kama ilivyoripotiwa na mtandao wa 90min,Sterling na chelsea tayari wamesha kubaliana maslahi binafsi, pia vilabu hivyo viwili sasa vinakamilisha ada ya uhamisho ya mchezaji huyo. Imefahamika kwamba Chelsea wanalazimika kulipa takriban pauni milioni 50 kwa ajili ya kupata huduma ya Sterling, ambaye mkataba wake naa City unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Vyanzo vimeiambia 90min kwamba Sterling atafanyiwa vipimo vya afya ndani ya masaa 48 zijazo. Kisha atajiunga na kikosi cha Chelsea kilichopo ziarani nchini Marekani.

Sterling anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Blues katika utawala wa mmiliki mpya wa chelsea Todd Boehly, lakini mmiliki huyo ana nia ya kuendelea kuongeza wachezaji zaidi.

Boehly ana hamu ya kufanya Usajili wa kishindo na anafikiria kumnunua Cristiano Ronaldo, ambaye ameiambia Manchester United anataka kuondoka msimu huu wa majira ya joto na timu yeyote itakayo leta ofa nzuri kwa ajili yake yupo tayari kuondoka.

Chelsea pia wanachuana na Barcelona kuhusu  kuinasa saini ya Raphinha. Winga huyo wa Leeds anapendelea kuhamia Barca, lakini Chelsea wako tayari kumpeleka darajani ikiwa tu atabadili uamuzi wake.

Post a Comment

0 Comments