Ticker

6/recent/ticker-posts

Mayele Arejea Yanga Kimya Kimya

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


MSHAMBULIAJI wa Yanga Fiston Mayele amewasili kambini kimya kimya na kumaliza uvumi uliozagaa kwamba huenda akatimkia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Mayele amewasili kambini bila mbwembwe nyingi kama za wakati mwingine na hata ujio wake ulikuwa kimya kimya.

Hofu ilitanda kwa mashabiki wa Yanga baada ya kuwepo ukimya kwa straika huyo huku wenzake wakiwa wameanza kambi yao huko Avic, Kigamboni, lakini mwamba huyo ametua kuanza maandalizi ya msimu mpya|.

Licha ya kwamba amechelewa kujiunga na wenzake straika huyo aliyemaliza ligi akiwa amefunga mabao 16, akiwa kwao DR Congo kwenye mapumziko alikuwa akiendelea kujifua kwa programu maalumu ya mazoezi aliyopewa na mwalimu Nasreddine Nabi na akawa akirekodi video kuonyesha anachokifanya hatua kwa hatua.

Hiyo inamaanisha kwamba kambini ataendelea pale walipo wenzake sababu hajapitwa .

Yanga imeingia kambini Julai 22 na Jumamosi walianza mazoezi tayari kwaajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi inayotarajiwa kuanza Agosti 17, mwaka huu.

Mapema akiwa bado nchini Congo Mayele aliiambia Mwanaspoti amesema alikuwa nje ya kambi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

“Pamoja na kuwa nje ya kambi nimefanya mazoezi kama kawaida ni baada ya kocha kunitumia programu ambayo inaniweka fiti ili nikiungana na timu niendelee na pale walipo wao,” alisema na kuongeza;

“Mimi bado ni mchezaji halali wa Yanga na nipo pamoja na timu kuhakikisha tunatetea mataji yetu tuliyoyatwaa msimu uliopita.”

Wakati Mayele alipokuwa nchini Congo wachezaji wenzake raia wa nchi hiyo, Jesus Moloko, Heritier Makambo, Djuma Shabani, Joyce Lomalisa wote walikuwa kambini mapema na wanaendelea na mazoezi.

Kuhusu mazoezi yanayoendelea, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema wachezaji walifanya mazoezi ya ‘gym’.

Post a Comment

0 Comments