Ticker

6/recent/ticker-posts

Neymar akabiliwa na kesi ya ulaghai Barcelona

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

•Neymar ​​anakabiliwa na kesi ya madai ya ukiukwaji wa taratibu za uhamisho kutoka Brazil kwenda Barcelona.

•Marais wawili wa zamani wa Barcelona, ​​Josep Maria Bartomeu na Sandro Rosell, pamoja na wazazi wa Neymar wanakabiliwa na madai hayo.Miaka tisa baada ya mwanasoka Neymar kuhama kutoka Brazil kwenda Barcelona,​​anakabiliwa na kesi ya madai ya ukiukwaji wa taratibu za uhamisho huo.

Katika sakata hilo ambalo limedumu kwa miaka mingi, mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye sasa anachezea Paris Saint-Germain anatuhumiwa kwa udanganyifu na ufisadi.

Kesi hiyo itafanyika kwa wiki mbili kuanzia tarehe 17 Oktoba, mwezi mmoja kabla ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Watu wengine kadhaa pia watashtakiwa .

Marais wawili wa zamani wa klabu ya soka ya Barcelona, ​​Josep Maria Bartomeu na Sandro Rosell, pamoja na wazazi wa Neymar wanakabiliwa na madai sawa, kulingana na ripoti za Uhispania.

Wale wote waliohusika katika kesi hiyo kwa muda mrefu wamekanusha madai hayo, yaliyotolewa na mfuko wa uwekezaji wa DIS, ambao ulidai kuwa ulikuwa na haki ya kupata 40% ya ada ya uhamisho ya Neymar 2013 alipoondoka klabu ya Santos ya Brazil.

Post a Comment

0 Comments