Ticker

6/recent/ticker-posts

Manchester United na Ajax wamethibitisha makubaliano juu ya uhamisho wa Lisandro Martinez

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Manchester United wamethibitisha kukubaliana na Ajax juu ya uhamisho wa Lisandro Martinez.

Ajax wamethibitisha kwamba United italipa €57.37m (£48.8m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambayo huenda ikapanda hadi kufikia €67.37m (£57.4m).


Muargentina huyo anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na United chini ya kocha Erik ten Hag, baada ya Tyrell Malacia na Christian Eriksen.

Martinez alihusishwa sana na Arsenal msimu huu wa majira ya joto, lakini aliachana na mpango wa The Gunners na kuamua kuungana na meneja wake wa zamani.

Taarifa kutoka Man Utd ilisema: "Manchester United inafuraha kutangaza kuwa imefikia makubaliano na Ajax kuhusu uhamisho wa mlinzi wa kimataifa wa Argentina Lisandro Martinez, baada ya kufaulu vipimo vya afya, masilahi binafsi kukamilika, na kibari cha kufanyia kazi kipo tayari."

Ajax walitoa taarifa kuthibitisha ada ya uhamisho: "Ajax na Manchester United wamefikia makubaliano ya uhamisho wa Lisandro Martínez," ilieleza.

Martinez Pamoja na mchezaji mwenza Christian Eriksen, hawataweza kujiunga na kikosi cha Man Utd kilichopo ziarani nchini Australia kwa ajili ya  ya kujiandaa na msimu mpya.

United wanaendelea na usajili kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwezi ujao, wanaendelea kufanyia kazi makubaliano ya kumleta Frenkie de Jong kutoka FC Barcelona.

Post a Comment

0 Comments