Ticker

6/recent/ticker-posts

Chelsea Wampandia Dau Matthijs de Ligt

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Bayern Munich na Chelsea waendelea kuvutana juu ya usajili wa Matthijs de Ligt, Chelsea wasema wapo tayari kumpeleka darajani kwa €100m.


Bayern Munich wanaimani wapo katika nafasi nzuri ya kumsajili mlinzi wa kati wa klabu ya Juventus Matthijs de Ligt, licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa Chelsea ambayo pia imeonyesha nia yakutaka kumsajili mchezaji huyo.

Matthijs de Ligt amechangua kuondoka Turin majira haya ya kipindi cha joto baada ya mazungumzo na waajili wake kugonga mwamba, kisa kikiwa nyongeza ya mshahara, de Ligt anataka aongezewe mshahara lakini waajili wake hawapo tayari kufanya hivyo na hiyo inawapa mwanga Bayern na Chelsea ambao wote wanahitaji huduma ya mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi bado anamkataba wa miaka miwili na waajili wake hivyo yeyote anaye muhitaji awe tayari kulipa kiasi kisicho pungua pauni milioni 77 ambacho juventus walitumia kumnunua mchezaji huyo kutoka Ajax mwaka 2019.

Juventus wanalazimika kumuuza mchezaji huyo msimu huu na wamepanga kumuuza si chini ya pauni milioni 84 ambazo zitamfanya de Ligt kushikilia rekodi ya kuwa beki ghari zaidi duniani.

Chelsea wapo tayari kulipa kiasi hicho cha fedha ili kuboresha safu yao ya ulinzi kufuatia walinzi  Antonio Rudiger na Andreas Christensen wote kuondoka baada ya mikataba yao kumalizika.

Bayern Munich wanaamini de Ligt anapendelea zaidi kujiunga nao baada ya kuvutiwa na mwongozo wa klabu hiyo alio upata kutoka kwa wakala wake baada ya kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa masuala ya Michezo wa Bayern "Hasan Salihamidzic" na kocha mkuu wa timu hiyo Julian Nagelsmann.

Kwingineko,Chelsea bado wanaendelea na harakati za Usajili wa Nathan Ake na Jules Kounde, ambao wote ni mabeki wa kati.


Post a Comment

0 Comments