Ticker

6/recent/ticker-posts

Ceasar Manzoki Asaini Simba Miaka miwili

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Manzoki Asaini Simba Miaka miwiliMABOSI wa Simba hawataki utani. Baada ya kuwasapraizi mashabiki kwa kufanya ishu ya kocha mkuu mpya kimyakimya kabla ya kumtangaza Zoran Manojlovic, nguvu zimehamia kwa wachezaji na juzi wameshusha straika mpya na fasta kumsainisha usiku mwingi.

Kama ulidhani mabosi wa Simba wamelala kwenye ishu za usajili umekosea, wamemalizana na kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Uganda, Ceasar Manzoki.

Simba imefanikiwa kumsajili  Manzoki anayecheza Vipers, Mabingwa wa Uganda kwa mkataba wa miaka miwili kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kinaeleza mazungumzo ya Manzoki na mabosi hao yameenda vizuri na juzi usiku alisaini mkataba na kuondoka usiku huohuo.Alitua nchini kimya kimya na kufichwa kwenye hoteli moja iliyopo katikati ya Dar es Salaam.

Chanzo hicho cha kuaminika kinaeleza Manzoki alikutana na mabosi hao wa Simba na kukubaliana kila kitu na ataanza kazi ya kuitumikia wikichache zijazo kama Moses Phiri.

Manzoki baada ya kumaliza jambo hilo alichukua ndege na kurudi Uganda kimya kimya bila ya kutaka mtu yeyote afahamu jambo hilo hadi hapo Simba itakapokuja kumtambulisha.

Post a Comment

0 Comments