Ticker

6/recent/ticker-posts

Nasreddine Nabi: Nani Abaki Kati Ya Chico Ushindi na Jesus Moloko

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Nasreddine Nabi: Nani Abaki Kati Ya Chico Ushindi na Jesus Moloko  

MAWINGA wa Yanga, Chico Ushindi na Jesus Moloko wamemtikisa Kocha, Nasreddine Nabi .

Anaumiza kichwa kufanya maamuzi ya nani wa kuachwa kutegemea na viwango watakavyoonyesha kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Coastal Union.

Yanga na Coastal Union zitacheza fainali hiyo Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. 

Awali Chico ndiye aliyeanza kuwa katika mtego huo wa Nabi aliyemtaka mchezaji huyo aamke kutoka usingizini na kupambana ili ajihakikishie kubaki.

Winga huyo kwenye mechi tatu za mwisho ameonyesha kiwango kizuri, huku akifunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union. 

Kocha Nabi alisema kuwa atawaomba viongozi waangalie namna gani wataendelea na Chico kwani anafanya vizuri na hilo baada ya kupona kwa asilimia zote.

“Chico alikuwa hachezi sana kwa sababu ya majeraha ambayo yalikuwa yanamsumbua, amepona na sasa anacheza, imani yangu atakuwa bora zaidi ya sasa,” alisema Nabi. 

Upande wa Moloko yupo kwenye kuti kavu zaidi baada ya kutoonyesha kiwango cha kuvutia lakini kinachombeba mpaka sasa ni ubora wake alioonyesha kwenye mechi za nyuma.

Lakini Mwanaspoti linajua Yanga itaachana na mmoja kati ya hao ili kupata nafasi ya kununua staa mpya. 

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha allipotafutwa azungumzie jambo hilo simu yake iliita bila kupokelewa.

Je, Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi

Post a Comment

0 Comments