Ticker

6/recent/ticker-posts

Barcelona wana uhakika wa kuwasajili Cesar Azpilicueta & Marcos Alonso licha ya kumwania Jules Kounde

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Barcelona wanaendelea na mazungumzo na Chelsea kuhusu usajili wa mabeki Cesar Azpilicueta na Marcos Alonso, Barca wanaamini kwamba makubaliano kuhusu wachezaji hao yatafikiwa hivi karibuni.

Pande hizo mbili zimekuwa zikivutana katika usajili wa beki wa kati wa Sevilla, Jules Kounde, ambaye amekubali kuhamia Chelsea lakini ame badili maauzi yake baada ya Barcelona kuingilia kati dili hilo.

Ripoti kutoka kwingineko zimesema kwamba Chelsea inaweza kusitisha mazungumzo na Barcelona ya kuwauzia Azpilicueta na Alonso kama kitendo cha kulipiza kisasi kwa kuingiliwa kati kwenye dili la beki Jules Kounde, Ingawa mbaka sasa pande hizo mbili bado zinaendelea kuwasiliana kuhusu makubaliano ya wachezaji hao mawili.

Maslahi binafsi kati ya mabeki hao wawili na barcelona yamekamilika na vilabu hivyo viwili sasa vinajadili ada ya uhamisho. Azpilicueta na Alonso wako katika miezi 12 ya mwisho ya mikataba yao.

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amekiri hadharani kusikitishwa kwake kuwapoteza kwa pamoja Azpilicueta, Andreas Christensen na Antonio Rudiger kwenye msimu huu wa usajili, na vyanzo vya karibu  vimethibitisha kuwa Tuchel amemhakikishia nahodha huyo wa The Blues kwamba bado anampango nae Stamford Bridge kwa msimu ujao.

Hata hivyo, Azpilicueta amefurahishwa na ofa ya Barcelona ya kumpa mkataba wa muda mrefu na chelsea wamesema hawatamlazimisha Azpilicueta kusalia klabuni hapo ikiwa atahitaji kuondoka.


Post a Comment

0 Comments