Ticker

6/recent/ticker-posts

Barcelona wanakaribia kumsajili Jules Kounde


Barcelona wanaamini kwamba wamefanya kila linalo wezekana kuipiku Chelsea katika mbio za kuinasa saini ya beki wa kati wa Sevilla Jules Kounde.

The Blues walidhani wameshinda mbio za kumnasa Mfaransa huyo mwishoni mwa juma lililopita baada ya kukubaliana ada ya usajili na Sevilla na ikiwemo makubaliano binafsi na mchezaji huyo, lakini Barcelona wakaingilia kati dili hilo  na sasa mchezaji huyo amebadili mawazo anataka kujiunga na Barca.

Barca wameshakubaliana kila kitu na Kounde na sasa wapo katika mazungumzo ya kuwashawishi Sevilla wakubali ofa yao, na vyanzo vya karibu vimethibitisha kuwa dili hilo linakaribia kukamilika.

Barcelona wamekubali kutoa dau la €50m, pamoja na nyongeza ya €10m zaidi, walilokuwa wanataka Sevilla kwa ajili ya mlinzi huyo ingawa mpango wa malipo bado haujafanyika, lakini dili hilo linakaribia kukamilika. 

Huku Kounde akionekana kuwakacha, Chelsea tayari wameanza kutafuta wachezaji mbadala,ambapo Wesley Fofana wa Leicester naye ameongezwa kwenye orodha ya wachezaji wanao waniwa na chelsea, wengine ni pamoja na Pau Torres wa Villarreal, Josko Gvardiol wa RB Leipzig, Milan Skriniar wa Inter, Presnel Kimpembe wa PSG. na wachezaji wawili wa Bayern Munich Dayot Upamecano na Benjamin Pavard.

Barcelona mbaka sasa tayari wameshaipiku Chelsea katika mbio za kumsajili Raphinha, huku wakimchukua Andreas Christensen kwa uhamisho huru na kufanikiwa kumshawishi Ousmane Dembele kukataa kuhamia Stamford Bridge na kufanikiwa kumsainisha mkataba mpya.

Hata hivyo chelsea na barcelona bado hawajamalizana, kwa sababu Barcelona wanawahitaji Cesar Azpilicueta na Marcos Alonso kutoka Chelsea na mazungumzo kuhusu makubaliano ya wachezaji hao mawili bado yanaendelea.

Kwa upande wa Sevilla, tayari wameshaanza kutafuta mbadala wa Kounde na sasa wanamuwinda Benoit Badiashile wa Monaco.

Post a Comment

0 Comments