Ticker

6/recent/ticker-posts

Aziz Ki, Bernard Morrison Waanza mazoezi rasmi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KIKOSI cha Yanga kimeanza rasmi mazoezi jana kujiandaa na msimu mpya ikiwemo mechi dhidi ya Simba Agosti 13. Stephane Aziz KI na Bernard Morrison ‘BM3’ ndiyo wachezaji wa kwanza kabisa kuripoti kambini na kubeba jukumu la kuwapokea wachezaji waliokuwa mapumziko walioripoti juzi.


Morrison na Ki wamesajiliwa dirisha kubwa la usajili na mara baada ya kutua nchini hawakurudi makwao kama ilivyokuwa kwa Joyce Lomalisa, Gael Bigirimana na Lazarous Kambole ambao walirudi kujipanga.

Yanga ilitangaza wachezaji wake kuanza kambi ya kujiandaa na msimu mpya Julai 22 na tayari wazawa wameingia kambini huku nyota wa kigeni wakikamilika jana.

Akizungumza, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ambaye ni miongoni mwa wanachama waandamizi, alisema wachezaji wameanza kuingia kambini juzi kwa mujibu wa ratiba ilivyokuwa imepangwa na jana jioni walianza mazoezi.

Alisema Morrison aligeuka mwenyeji kwa kuwakaribisha mastaa ambao wameanza kuingia kambini hasa wazawa ambao hawajaitwa Taifa Stars.

“Kama kawaida ya Morrison na uchangamfu wake amekuwa akiwakaribisha wachezaji walioanza kuingia kambini jana kutokana na kuwa miongoni mwa wachezaji waliotangulia kufika,” alisema na kuongeza;

“Siwezi kutaja idadi ya wachezaji waliopo hadi sasa kambini kwasababu muda bado upo na wachezaji wanaendelea kujiunga na wenzao tayari kwa maandalizi ya msimu mpya, timu inatakiwa kukamilika jioni tutaanza mazoezi.”

Naye winga wa timu hiyo, Jesus Moloko alisema ameona sajili mbili zilizofanyika katika nafasi anayocheza anakazi kubwa ya kufanya kwenye uwanja wa mazoezi kuhakikisha aondoki kikosini.

“Ni muda wa kila mchezaji kuonyesha uwezo wake kipindi hiki ambacho usajili wa wachezaji wapi umeongezeka ili kujihakikishia nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza ujio wa wachezaji wanaocheza nafasi moja na mimi utaniongeza chachu ya ushindani.” alisema.

Moloko ambaye aliwasili usiku wa kuamkia leo, alisema kila mchezaji anaumuhimu wake kiwanjani na kocha Nasreddine Nabi ndiye mwenye maamuzi ya mwisho nani acheze na nani aanzie benchi atatumia muda wake mwingi kuonyesha uwezo mazoezini ili kumshawishi aweze kuendelea kumuamini. Yanga itatambulisha mastaa wake, Agosti 6, Uwanja wa Mkapa.

Post a Comment

0 Comments