Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi Za Usajili: Ronaldo Kutolewa Kwa Mkopo; Antoine Griezmann Kuuzwa

Tetesi Za Usajili: Ronaldo Kutolewa Kwa Mkopo; Antoine Griezmann Kuuzwa

Manchester United wako tayari kumuachia Cristiano Ronaldo kwa mkopo katika msimu huu wa majira ya joto  kwa timu yeyote itakayo muhitaji. Mshambulizi huyo wa Ureno anataka kuondoka Old Trafford lakini bado hakuna klabu iliyo onyesha nia ya kumuhitaji.

Klabu ya Atletico Madrid imemuweka sokoni mshambuliaji wake Antoine Griezmann kwa lengo  la kupata fedha za nyongeza ili kumnunua Ronaldo.

Chelsea na Inter tayari wamekamilisha makubaliano juu ya Romelu Lukaku kutumia msimu wa pili wa mkopo nchini Italia.

Youri Tielemans bado anawindwa na Arsenal. Mbelgiji huyo hataki mkataba mpya Leicester na amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa, ingawa The Gunners bado hawajawasilisha ofa.

Ripoti kutoka Uhispania zinadai kwamba Jules Kounde hivi karibuni atakuwa mchezaji wa Barcelona, ​​ingawa Chelsea bado wanaamini kuwa dili hilo litakamilika.

Jurgen Klopp anasema Liverpool 'tuna kikosi kinacho jitosheleza' kwa msimu ujao na haoni kwamba klabu hiyo itasajili tena msimu huu wa majira joto.

Eder Militao ametia saini mkataba mpya na Real Madrid, ambao wameingiza kipengele cha timu itakayo muhitaji iwe tayari kumnunua kwa euro milioni 500 katika mkataba huo.

Bayern Munich wamefikia makubaliano na Rennes kumsajili Mathys Tel mwenye umri wa miaka 17, huku Usajili huo ukitarajiwa kukigharimu takriban €28.5m.

Paris Saint-Germain wanakaribia kumnasa beki wa kulia wa RB Leipzig Nordi Mukiele baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano.

Charles De Ketelaere anaye takiwa na Leeds na AC Milan aliachwa nje katika kikosi cha Club Brugge katika mechi yao ya kwanza ya ligi msimu huu dhidi ya Genk Jumapili.

Nice wamemgeukia Kipa wa Leicester Kasper Schmeichel baada ya kushindwa kumsajili Yann Sommer kutoka Borussia Monchengladbach.

Everton wapo tayari kuachana na Mshambuliaji Dele Alli ikiwa ni mwaka mmoja tangu wamchukue kutoka Tottenham.

Post a Comment

0 Comments