Ticker

6/recent/ticker-posts

Augustine Okrah Aanza Kwa Mabao Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Augustine Okrah amewaambia mashabiki wa klabu yake wategemee magoli zaidi kutoka kwake.

Okrah amefunguka hayo mara baada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na Simba katika mechi ya majaribio waliyoipiga dhidi ya Ismaily nchini Misri jana Julai 17, 2022.


“Nampongeza kocha kwa kunipa nafasi ya kucheza na kufunga bao la kwanza nikiwa na Simba SC. Mashabiki wa Simba wategemee magoli zaidi kama ambavyo nimekuwa nikifanya siku zote,” alisema Okrah.

Simba imeweka kambi katika mji wa Ismailia ikijiandaa na mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya watani wao wa jadi Yanga inayotarajiwa kupigwa Agosti 13, 2022.

Post a Comment

0 Comments