Ticker

6/recent/ticker-posts

Tarik Sektioui Kurith Mikoba Ya Pablo Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapaTarik Sektioui Kurith Mikoba Ya Pablo Simba, baada ya kimya kirefu kuhusu nani wa kumrithi aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya simba sasa mambo yawekwa wazi baada ya michakato kukamilika.

Imeelezwa  kuwa suala la kocha mpya ndani ya Simba limeisha, baada ya kuwa kwenye mchakato mrefu ambao mwisho wa siku ni Tarik Sektioui atapewa mikoba hiyo.

 Sektioui ni raia wa Morocco, ambaye amefundisha klabu nyingi nchini humo ikiwemo RS Berkane ambayo aliinoa msimu wa 2019/2020 na kuiwezesha kutwaa Kombe la Shirikisho la CAF.

 Chanzo chetu kutoka Simba, kimeeleza kuwa mchakato wa kumpata kocha huyo umeendeshwa na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Mwenyekiti wa Bondi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’, hivyo muda wowote kuanzia sasa atawekwa hadharani.

“Naomba ufahamu tu kwamba, hadi muda huu tunaozungumza kama hakuna mabadiliko, basi kocha tayari ameshatua hapa nchini, maana makubaliano ni kwamba atafika muda wowote.

 “Kocha alitakiwa kufika na kusaini ili angalau ashuhudie michezo miwili ya mwisho ya ligi, mipango ambayo nina imani nayo itakuwa imefanikiwa,” kilisema chanzo hicho.

Kocha huyo anakuja kuchukua nafasi ya Pablo Franco raia wa Hispania ambaye alifungashiwa virago Mei 31, mwaka huu baada ya kushindwa kufikia malengo ya klabu ambapo Simba imelikosa taji la Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports, huku Kombe la Shirikisho Afrika ikiishia robo fainali.

Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Kaimu Kocha Seleman Matola ambaye jana alionja joto ya jiwe kwa timu hiyo kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Post a Comment

0 Comments