Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais wa Urusi Vladimir Putin Kufanya Ziara ya Kwanza Nje ya Urusi Tangu Avamie Ukrain

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa pamoja na Rais wa China Xi Jinping

RAIS wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza nje ya Urusi tangu Taifa lake lifanye uvamizi kwa nchi ya Ukraine.

Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Habari cha Rossiya 1 cha Ikulu ya Urusi, Pavel Zarubin amesema Rais Putin atatembelea mataifa madogo mawili yaliyopo Bara la Asia ambayo yalikuwa chini ya Umoja wa Kisovieti na mbayo yana mlengo sawa na Taifa la Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na Rais wa Indonesia Joko Widodo

Zarubin ameyataja mataifa hayo kuwa ni Tajikistan pamoja na Turkmenistan na baada ya hapo anatarajiwa kukutana na Rais wa Indonesia Joko Widodo kwa ajili ya mazungumzo jijini Moscow.

Ziara ya mwisho ya Rais Putin nje ya mipaka ya Urusi ilikuwa mapema mwezi Februari ambapo alikutana na Rais wa China Xi Jinping ambapo walisaini mkataba wa urafiki usiokuwa na mipaka ikiwa ni masaa machache kabla ya wote kuungana kwenye sherehe ya ufunguzi wa mashindano ya Olimpic ya majira ya baridi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin

Akiwa ziarani barani Asia Putin anatarajiwa pia ukutana na viongozi wa nchi za Azerbaijan, Kazakhstan pamoja na Iran.

Mnamo Februari 24 Urusi iliivamia Ukraine na kusababisha maafa makubwa nchini humo ikiwemo kuua maelfu ya watu, kusababisha mamilioni ya watu kukimbia makazi yao na pia kusababisha vikwazo vikali kutoka Mataifa ya Magharibi.

Post a Comment

0 Comments