Ticker

6/recent/ticker-posts

Raphinha kutua Chelsea kwa pauni mil 65

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Raphinha kutua Chelsea kwa pauni mil 65
KLABU ya Chelsea ipo katika nafasi nzuri ya kumsajili winga wa Leeds United, Raphinha baada ya kutoa ofa ya pauni milioni 65 ikijumuisha nyongeza ya mchezaji mmoja katika dili hilo ili kukamilisha uhamisho wa nyota huyo wa kimataifa wa Brazil.

The Blues tayari walikuwa wakifuatilia hali ya mchezaji huyo na ghafla wamepiga hatua mbele kwenye mbio hizo, ambazo pia zipo Barcelona na Arsenal.

Barcelona pamekuwa mahali anapopendelea Raphinha hadi sasa, lakini mtandao wa 90min umefichua kwamba, Wakatalunya hao wanakabiliwa na ukata.

Fedha zimesalia kuwa wasiwasi kwa klabu hiyo ya Hispania kuhusu uhamisho wa msimu huu wa joto na biashara itategemea mauzo ya wachezaji wengine.

Awali iliilezwa kuwa Arsenal pia walikuwa wamewasilisha ofa kwa Mbrazil huyo katika jaribio la kutaka kumsajili, lakini ofa hiyo ikakataliwa na Leeds.

Washikabunduki sasa wanafikiria iwapo waongeze ofa yao kwa kuzingatia uhamisho wa Chelsea.

Raphinha alifanikiwa kufunga mabao 11 na kutoa pasi tatu za mabao kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, na kuinusuru Leeds na mwenendo mbovu wa matokeo.

Chelsea tayari iko kwenye mazungumzo na Ousmane Dembele, ambaye anatazamiwa kuwa mchezaji huru baada ya siku chache mkataba wake Barcelona utakapomalizika. 

Majadiliano pia yanaendelea na winga wa Manchester City, Raheem Sterling ili kumsajili majira haya ya joto kule Stamford Bridge.

Post a Comment

0 Comments