Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga, Kaizer wakanusha dili la Mayele

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Yanga, Kaizer wakanusha dili la Mayele


Wakati taarifa zikidai mshambuliaji kinara wa mabao ndani ya klabu ya Yanga, Fiston Mayele yuko mbioni kutimkia Kaizer Chiefs klabu zote mbili zimekanusha taarifa juu ya dili hilo.

Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema hakuna kitu kama hicho juu ya Mayele kuondoka.

"Hizo ni taarifa za uongo huku ndani kwetu hakuna kitu cha namna hiyo, nilishatoa msimamo wa klabu kwamba Mayele hauzwi kwa gharama yoyote," amesema Senzo.

Aidha Senzo ameongeza kwamba kwasasa mshambuliaji huyo aliyemaliza wa pili katika ufungaji wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 16, akili yake inajiandaa na mchezo wa Fainali ya Azam Shirikisho dhidi ya Coastal Union itakayopigwa Julai 2 jijini Arusha.

Naye mtoto wa mmiliki wa klabu ya Kaizer Chiefs Kaizer, Motaung Junior amekanusha taarifa hizo kupitia akaunti yake ya Twitter akiandika kwa kifupi "msimu wa habari za kipuuzi unaendelea"

Post a Comment

0 Comments