Ticker

6/recent/ticker-posts

Neymar Kuikimbia PSG Msimu Huu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Neymar, Mshambuliaji nyota wa kimataifa anachezea klabu ya PSG Nchini Ufaransa anatarajiwa kuachana na klabu hiyo msimu huu wa joto baada ya tetesi za kwamba amechukizwa na mkuu wa PSG kwa kusema kiwango chake kimepunguwa kwa msimu ulio pita.

Miononi mwa klabu zinazo mmendea ni Chelsea ambao ni miongoni mwa chaguo pekee la uhamisho wa nyota wa Paris Saint-Germain Neymar msimu huu wa joto.

Yamesemwa hayo wakati ambapo nyota huyo anaripotiwa kufikiria mustakabali wake baada ya kukasirishwa na mkuu wa PSG Nasser Al-Khelaifi akidokeza kuwa kiwango chake kilikuwa chini ya kiwango msimu uliopita.

Kwa mujibu wa RMC Sport, mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil anafikiria kuondoka Parisi msimu huu, miaka mitano baada ya uhamisho wake uliovunja rekodi ya dunia wa Paundi Milioni 198 kutoka Barcelona.

Ripoti za mwezi huu zilidai kuwa PSG wako tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa bei inayofaa huku wakipanga kumjenga upya majira ya kiangazi.

Timu tatu za Premier League Manchester United, Chelsea na Newcastle ndizo timu pekee zenye pesa za kutosha kumsajili Neymar

Je, Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments