Ticker

6/recent/ticker-posts

Stephane Aziz Ki kusaini mkataba mpya Young Africans

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kuna uwezekano mkubwa wa Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans kumsainisha mkataba mpya kiungo mshambuliaji kutoka Burkina Faso Stephane Aziz Ki.

Mkataba wa sasa wa Kiungo huyo unatarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, akiitumikia Young Africans kwa msimu wa pili sasa, baada ya kusajiliwa mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea ASC Mimosas ya Ivory Coast.

Chanzo kutoka ndani ya Young Africans kimeeleza kuwa, mabosi wa timu hiyo wameanza mchakato wa kumpa mkataba mpya staa huyo mapema ili kuepuka uwezekano wa kumpoteza bure mwisho wa msimu.

“Kwa uwezo ambao anauonesha Aziz msimu huu, ni wazi litakuwa jambo la ajabu kuona tunampoteza bure mwishoni mwa msimu, hivyo uongozi umeanza haraka mchakato wa mazungumzo ya awali ya kumpa mkataba mpya ambao unatarajiwa kuwa na thamani kubwa kuliko ule ambao alisaini wakati anakuja. Tunafahamu kuna baadhi ya timu kubwa nazo zimeanza kumfuatilia,” kimesema chanzo hicho.

Maxi awataka wachezaji wenzake kuto bweteka

Akizungumzia suala la uboreshaji wa mikataba ya wachezaji wa timu hiyo, Rais wa Young Africans, Injinia Hersi Said, amesema: “Suala lolote la mikataba linategemea na mahitaji ya kocha, hivyo tutahakikisha tunatimiza matakwa ya kumbakisha mchezaji yeyote na kuongeza nguvu kwa kuleta mastaa wapya pale inapohitajika,”

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, Rodgers Gumbo, amesema: “Malengo yetu ni kuhakikisha tunakuwa na timu ambayo itaandika historia katika mashindano ya kimataifa, hivyo tuko tayari kulipa gharama yoyote kufanikisha hilo.”

Post a Comment

0 Comments