Ticker

6/recent/ticker-posts

Aubin Kramo wa Asec Mimosas atua Simba Sc

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KLABU ya Simba Sc imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Aubin Kramo kutoka Asec Mimosas kwa mkataba wa miaka miwili.

Kramo (27) raia wa Ivory Coast ana uwezo wa kucheza winga zote mbili na kucheza namba 10.

Aubin Kramo anakuwa mchezaji wa pili wa kigeni kutambulishwa Simba Sc baada ya Uongozi wa klabu hiyo kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Willy Essomba Onana (23) raia wa Cameroon kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba SC imemsajili Onana  kwa dola za kimarekani 200,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Milioni 495 na huku akipokea Mshahara wa shilingi milioni 19 kwa Mwezi.

Onana amesajiliwa kutoka Rayon Sports ya Rwanda ambapo msimu uliopita ameibuka mchezaji bora wa ligi kuu nchini humo (MVP).

PICHA: Willy Essomba Onana atambulishwa Simba SC rasmi

Onana ni mchezaji mwenye kipaji na uwezo mkubwa wa kucheza nafasi za mbalimbali uwanjani winga zote mbili pia anaweza kumudu nyuma ya mshambuliaji (namba 10) pia mshambuliaji kivuli (False number nine).

Msimu uliopita Onana aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu nchini Rwanda baada ya kufunga mabao 16 na kusaidia kupatikana kwa mengine matano (Assist)

Onana ndiye ingizo jipya la kwanza kikosini kwetu ikiwa ni sehemu ya maboresho kuelekea Msimu Mpya wa Ligi 2023/24.

Kupitia kurasa zake ya mitandao ya kijamii mshambuliaji Aubin Kramo amewashukuru viongozi wa Asec Mimosas kwa kuandika ujumbe huu

"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa klabu kwa kuwa na imani na uwezo wangu na kunipa nafasi hii ya kuiwakilisha Simba sc. Nimenyenyekea na kuhamasika kufanya kazi bila kuchoka ili kuchangia mafanikio ya timu na kuzingatia maadili ya klabu."


Post a Comment

0 Comments