Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yamuwinda Kouassi Attohoula kutoka ASEC Mimosas

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Yanga ipo kwenye mawindo ya saini ya Beki  wa kulia kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast, Kouassi Attohoula, ambaye atachukuwa nafasi ya Mamadou Doumbia.

Yanga inajiandaa kumsajili beki huyo ikiwa ni sehemu ya kukiboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa, ambapo wamedhamiria kufanya makubwa zaidi ya ilivyokuwa msimu huu 2022/23.

Mmoja wa mabosi wa Yanga amesema kuwa klabu hiyo inakamilisha taratibu za kuipata saini ya beki huyo raia wa Burkina Faso mwenye uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi sambamba na kupiga krosi safi za mabao.

Djigui Diarra atoa kauli ya kishujaa

Bosi huyo amesema kuwa, kama dili hilo likikamilika kwa asilimia mia moja, basi upo uwezekano mkubwa wa Doumbia kumpisha Attohoula atakayekuja kucheza nafasi ya beki wa kulia.

Ameongeza kuwa viongozi wa Yanga wanaangalia uwezekano wa kumtoa kwa mkopo Doumbia katika msimu ujao kwenye timu yake aliyokuwa anaichezea huko nyumbani kwao Mali.

“Kama dili la usajili la Attohoula ambaye ni beki wa Asec Mimosas kutua Yanga, basi safari ya Doumbia itakuwa imewadia ya kuondolewa ili ampishe huyo beki wa pembeni.

“Attohoula ni kati ya wachezaji walionyesha kiwango bora katika msimu katika Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na Asec Mimosas.

“Na kocha Nabi (Nasreddine) ndiye anayeonekana kuhitaji saini ya Attohoula baada ya kuvutiwa naye baada ya kumuona katika michuano hiyo mikubwa Afrika,” amesema bosi huyo.

Akizungumzia hilo la usajili Nabi amesema: “Usajili wangu utakuwa na baadhi ya maingizo mapya machache katika kikosi changu, nitasajili mabeki wa pembeni, mawinga na washambuliaji kila sehemu wachezaji wawili.”

Post a Comment

0 Comments