Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga Yamtaka Feisal Salum Kuripoti Kambini Haraka

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

BAADA ya kupokea maamuzi ya marejeo ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kuhusu suala la mchezaji wake Feisal Salum Abdallah, klabu ya Yanga imemwandikia barua Feisal Salum kumtaka aripoti kambini haraka iwezekanavyo na kuendelea kuutumikia mkataba wake kama mchezaji halali wa Yanga mpaka tarehe 30, Mei 2024, kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.

Aidha, Klabu ya Yanga iko tayari kumpokea Feisal Salum na kumjumuisha kwenye kikosi, na kwa kuzingatia sera na utaratibu wa Klabu ya Yanga katika kuwaongezea mikataba wachezaji wake wanaofanya vizuri, Uongozi wa Yanga uko tayari kuendelea na mazungumzo na Feisal Salum Abdallah na wawakilishi wake juu ya kuboresha mkataba wake, kama wataridhia.

Mwisho, Klabu ya Yanga inapenda kuutaarifu umma kwamba iko tayari kumruhusu Feisal Salum Abdallah kuondoka klabuni kwa kuzingatia matakwa ya mkataba na utaratibu wa sheria za uhamisho wa wachezaji zinazotambulika na TFF pamoja na FIFA. Ikiwa pia kuna klabu yoyote inahitaji huduma ya mchezaji huyu, klabu ya Yanga iko tayari kufanya mazungumzo wakati wowote.

Post a Comment

0 Comments