Ticker

6/recent/ticker-posts

Erling Haaland ni moto wa kuotea mbali

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

WINGA wa Manchester City, Jack Grealish amekiri Erling Haaland ni moto wa kuotea mbali kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao huku akisisitiza kushangazwa na alichoambiwa na kipa wa FC Copenhagen, Kamil Grabara baada ya straika huyo kumtungua mabao mawili katika mechi ambayo kikosi cha Pep Guardiola kilishinda 5-0 kwenye mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya juzi.

Grealish alisema: “Inashangaza sana kwakweli, sijawahi kushuhudia mtu wa aina hii katika maisha yangu, baada ya Haaland kufunga bao lake la pili, wakati natembea kurudi kati, kipa wa Copenhagen aliniambia ‘huyu Haaland sio sio binadamu wa kawaida’, nikawa nacheka tu.”

Baada ya kumshuhudia Haaland akifunga mabao mawili na kufikisha mabao 19 katika mechi 12 za michuano yote alizoitumikia City msimu huu, kocha Guardiola alizungumzia ishu ya mkataba ya staa huyo akikanusha madai kwamba una kipengele cha kununuliwa na timu yoyote siku za usoni, huku Real Madrid ikihusishwa.

Post a Comment

0 Comments