Ticker

6/recent/ticker-posts

Zlatan Ibrahimovic Aongeza Mkataba AC Milan

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic amerefusha muda wa kuhudumu kwake kambini mwa AC Milan ya Italia kwa mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

Ina maana kwamba mshambuliaji huyo raia wa Uswidi atakuwa bado akivalia jezi za mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) atakapofikisha umri wa miaka 41.

Ibrahimovic ambaye ataadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa mnamo Oktoba 2022, alifungia AC Milan mabao nane msimu wa 2021-22 na kuongoza kikosi hicho kunyanyua taji la Serie A baada ya kuwapiku wapinzani wao wakuu, Inter Milan.

Nyota huyo alifanyiwa upasuaji wa goti mnamo Mei 2022 na alitarajiwa kuwa nnje kwa kipindi cha miezi minane.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona, Manchester United na Paris Saint-Germain (PSG), alirejea AC Milan mnamo 2020 na akawasaidia kutwaa taji la Serie A mnamo 2021-22, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11.

Post a Comment

0 Comments