Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Usajili barani Ulaya: Ronaldo Atumiwa Ofa kubwa kutoka Saudi; Messi Kubakia PSG

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Tetesi za Usajili barani Ulaya:Ronaldo Atumiwa Ofa kubwa kutoka Saudi; Messi Kubakia  PSGKlabu moja ya nchini Saudia imetuma ofa ya €30m Ikitaka kumsajili Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo, ikiwa ni pamoja na Mkataba mnono. Gwiji huyo wa Ureno amewaambia waajiri wake wa sasa kuzingatia ofa zozote zinazomfaa katika msimu huu wa majira ya joto, lakini United inasisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi.

Paris Saint-Germain wanajiandaa kumuongezea mkataba Mshambuliaji wao Lionel Messi. Mshambulizi huyo mashuhuri yuko ndani ya miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake.

Kocha mkuu wa Barcelona Xavi amemwambia kiungo Frenkie de Jong kwamba huenda akauzwa kutokana na ugumu wa kifedha wa klabu hiyo, huku Man Utd wakiendelea kumuhitaji.

Winga wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele hatimaye atatia saini mkataba mpya Camp Nou siku ya Alhamisi kufuatia kipindi kirefu cha sintofahamu kuhusu mustakabali wake.

Lisandro Martinez ameweka wazi nia yake ya kutaka kujiunga na United baada ya kuikataa Arsenal, kwani anapendelea kuhamia Old Trafford,  United wamefikia makubaliano ya Awali na Ajax kwa ajili ya mchezaji huyo.

Jesse Lingard ambae ni mchezaji huru anaweza kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Man Utd Wayne Rooney huko D.C. United.

Baada ya kukamilisha usajili wa Raheem Sterling siku ya Jumatano, Chelsea wanakaribia kuinasa saini ya beki wa kati wa Napoli Kalidou Koulibaly - ambaye anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya hivi karibuni.

Chelsea pia wapo kwenye mazungumzo na Paris Saint-Germain kwajili ya beki Presnel Kimpembe.

Nathan Ake anakaribia kurejea Stamford Bridge, na Man City wanajiandaa kuziba nafasi yake kwa kumsajili chipukizi wa RB Leipzig Josko Gvardiol.

Winga Serge Gnabry anakaribia kusaini mkataba mpya Bayern Munich. Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal alikuwa akihusishwa na tetesi za kuhama baada ya kuwa kubakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Juventus wameelekeza nguvu zao kwa beki wa kati wa Villarreal, Pau Torres wakati wakijiandaa kwa maisha bila ya Matthijs de Ligt.

Real Madrid haitampa mkataba mpya mshambuliaji wao Marco Asensio katika msimu huu wa majira ya joto, lakini mchezaji huyo hayupo tayari kuondoka kwa sasa hivyo anaweza kuondoka bure katika kipindi cha miezi 12 ijayo baada ya mkataba wake kufika mwisho. Anapendelea kuungana na Jurgen Klopp katika klabu ya Liverpool baada ya mkataba wake na Madrid kwisha.

Newcastle wanajiandaa kutuma ofa ya mwisho kwa ajili ya kumsajili Moussa Diaby kutoka Bayer Leverkusen katika msimu huu wa majira ya joto.

Man City wako tayari kumruhusu mshambuliaji wao chipukizi Liam Delap kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha hili la usajili, na Tayari Southampton na Burnley wameonyesha nia ya kumuhitaji mshambuliaji huyo kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu.

Mchezaji nyota wa Aston Villa Carney Chukwuemeka ameachwa katika kikosi kilicho kwenda ziarani kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya baada ya nyota huyo kushindwa kusaini mkataba mpya. Vilabu kadhaa barani ulaya vimeonyesha nia ya kumuhitaji, huku Newcastle na Arsenal wakimfuatilia kwa Ukaribu.

Arturo Vidal ameondoka Inter na kurejea kwao Brazil kujiunga na Flamengo ya nchini Kwao , hiyo Inafungua njia kwa Paulo Dybala kujiunga na Nerazzurri.

Inter pia wanakaribia kuinasa saini ya beki wa kati Gleison Bremer kutoka Torino.

Post a Comment

0 Comments