Ticker

6/recent/ticker-posts

TFF Yatangaza Majina Ya Washidi Wa Tuzo Zao

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

TFF Yatangaza Majina Ya Washidi Wa Tuzo Zao

Sherehe za tuzo za Shirikisho la soka Tanzania (TFF), msimu wa 2021-22, zinatarajiwa kufanyika Julai 7 mwaka huu katika ukumbi wa Rotana Hotel, Dar es Salaam.

Tuzo za TFF zimegawanyika katika makundi mbalimbali, zikiwemo kikanuni za mashindano, binafsi za wachezaji na waamuzi, keshima na kiutawala zikihusisha wasimamizi wa mpira wa miguu na wadau wengine waliotoa mchango wao kwa mchezo huo.

Ukiachana na tuzo za kawaida zinazohusiana na mashindano kwa maana ya bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na wa nne, kutakuwa na tuzo binafsi 57, zikiwemo zile zinazotolewa kwa mtu zaidi ya mmoja, mfano seti bora ya waamuzi, kikosi bora cha Ligi Kuu ya Wanawake na kikosi bora cha Ligi Kuu Bara.

Pia kwa mara ya kwanza msimu huu katika sherehe za Tuzo za TFF, kutakuwa na Tuzo ya mchezaji Bora wa Ligi ya Championship na pia Mchezaji Bora wa First League. Miaka ya nyuma wachezaji hao walikuwa wanatunzwa mara baada ya mashindano husika kumalizika.

Mchanganuo wa Tuzo za TFF ni kama ifuatavyo:

Mshindi wa Pili wa Kombe la Shirikisho (ASFC) atakuwa kati ya Coastal Union na Yanga ambao watacheza fainali kesho Jumamosi Julai 2.

Bingwa wa kombe la Shirikisho la (ASFC) atakuwa Coastal Union au Yanga waliokuwa kwenye fainali kesho.

Tuzo ya mshindi wa tatu Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) itakwenda kwa Yanga Princess.

Mshindi wa Pili Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) tuzo itachukuliwa na Fountain Gate Princess.

Tuzo ya bingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) imechukuliwa na Simba Queens.

Kwenye Ligi Kuu Bara zawadi ya mshindi wa nne imekwenda kwa Geita Gold FC wakati Azam itachukua ya mshindi wa tatu huku Simba ikichukua ya mshindi wa pili na Yanga ikichukua ile ya bingwa.

Tuzo ya mfungaji bora wa ASFC itakwenda kwa Abdul Selemani (Coastal Union) mwenye mabao sita au Heritier Makambo (Young Africans) mwenye mabao matatu. Wawili hao timu zao ndio zimetinga fainali.

Tuzo ya mfungaji bora Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) itachukuliwa na Asha Djafar kutokea Simba Queens aliyemaliza msimu na mabao 27, wakati tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Bata imekwenda kwa George Mpole wa Geita aliyemaliza msimu na mabao 17.

Katika kipingele cha timu yenye nidhamu katika Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) inawaniwa na timu tatu kati ya Yanga Princess, JKT Queens na Alliance Girls.

Katika Ligi Kuu Bara tuzo yenye nidhamu inawaniwa na Tanzania Prisons, Yanga na Simba SC na mmoja kati ya hao ndio ataichukua.

Meneja bora wa uwanja inawaniwa na Sikitu Kilakala - Uwanja wa Azar Complex (Dar es Salaam) Mwaluka Modestus Uwanja wa Sokoine (Mbeya) na Godfrey Komba - Uwanja wa Manungu (Morogoro).

Kamishina bora Ligi Kuu Bara inawania na Abousufian Sillia kutokea Iringa, Abubakary Kazinja kutokea Kagera na Somoe Ng'itu - Dar es Salaam ambaye pia ni Mwanahabari wa michezo.

Seti Bora ya waamuzi Ligi Kuu Bara inawaniwa na wale waliyochezesha mechi kati ya Yanga na Simba, Simba na Yanga sambamba na mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga.

Mwamuzi msaidizi bora Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) inawaniwa na Zawadi Yusuph wa Dar es Salaam, Sikudhan Mkulungwa wa Njombe na Glory Tesha - Dar es Salaam.

Mwamuzi Msaidizi Bora Ligi Kuu ya Kuu Bara inawaniwa na Frank Komba - Dar es Salaam aliyechukua msimu uliopita, Mohammed Mkono wa Tanga na Janeth Balama kutokea Iringa.

Tuzo ya kocha Bora Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) inawania wa na Sebastian Nkoma wa Simba Queens, Masoud Juma wa Fountain Gate Princess na Edna Lema - Yanga Princess.

Kocha Bora Ligi Kuu Bara tuzo yake inawaniwa na Nasreddine Nabi wa Yanga, Fredy Minziro wa Geita Gold Juma Mgunda na Coastal Union.

Tuzo ya chipukizi bora Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) inawaniwa na Clara Luvanga wa Yanga Princess, Frida Gerald wa Fountain Gate Princess na Winfrida Charles - Alliance Girls.

Mchezaji bora chipukizi Ligi Kuu Bara inawania wa Dickson Mhilu wa Kagera Sugar, Tepsie Evance wa Azam na Richardson Ng'ondya wa Mbeya City.

Tuzo ya Fair Play Ligi Kuu Bara itatangazwa ukumbini, wakati ile ya mwamuzi bora Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) inawaniawa na Tatu Malogo wa Tanga, Amina Kyando wa Morogoro na Esther Adabert wa Singida.

Mwamuzi Bora Ligi Kuu Bara tuzo yake inawaniwa na Ramadhan Kayoko kutokea Dar aliyetwaa mara mbili mfululizo, Ahmed Arajiga kutokea Manyara na Elly Sasii wa Dar.

Tuzo ya kipa bora wa kombe la ASFC inawaniwa na Mohamed Mohamed wa Coastal Union, Djigui Diara wa Yanga na Beno Kakolanya kutokea Simba.

Wakati tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) inawaniwa na Gelwa Yona wa Simba Queens, Asha Mrisho wa Tiger na Caroline Rufa wa Fountain Gate Princess, wakati kipa bora wa Ligi Kuu Bara inawaniwa na Djigui Diara wa Yanga, Aishi Manula wa Simba na Khomein Abubakar wa Geita Gold.

Beki bora Ligi Kuu Bara inawaniawa na Djuma Shaaban wa Yanga, Henock Inonga wa Simba na Bakari Mwamnyeto wa Yanga wakati tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu Bara wamo, Yanick Bangala, Feisal Salum na Salumu Abubakary 'Sure Boy' wote wa Yanga.

Wakati tuzo ya Rais wa TFF, itatangazwa ukumbini kama ambavyo zitakuwa tuzo ya heshima, mchezaji Gwiji (The Legend Award) tuzo ya heshima (Women Footbail), goli Bora Ligi Kuu Bara, kikosi bora cha Ligi Kuu ya Wanawake na kikosi bora cha Ligi Kuu Bara.

Soma Pia Azam Fc Yamtangaza Mnigeria Isah Ndala

Tuzo ya mchezaji bora wa ASFC inawaniwa na Sopu wa Coastal Union, Feisal na Fiston Mayele wote wa Yanga wakati tuzo ya mchezaji bora wa SWPL inawaniwa na Asha Djafar wa Simba Queens, Amina Millal wa Yanga Prencesss na Fatma Issa wa Simba Queens.

Mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara inawaniwa na Inonga wa Simba, Bangala na Mayele wote wa Yanga wakati mchezaji bora wa Championship inawaniwa na Edward Songo wa JKT Ruvu, Kenani Mwelukilwa wa Kitayosce na Mohamed Haji wa Mashujaa.

Tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Daraja La Kwanza inawaniwa na Selemani Kibuta wa Alliance, Mohamed Hussein wa Capco Veteran na Yassin Mgaza wa Mbuni


Post a Comment

0 Comments