Ticker

6/recent/ticker-posts

Jezi Mpya Ya Yanga Msimu Ujao Inapatikana Kila Kona Ya Tanzania

Jezi Mpya Ya Yanga Msimu Ujao Inapatikana Kila Kona Ya Tanzania


Jana Julai 28,2022 Yanga imezindua JEZI mpya ambazo zinatarajiwa kutumika kwa msimu wa 2022/23.

Kwa mujibu wa Rais wa Yanga,Injinia Hersi Said amesema kuwa uzi huo kwa sasa unapatikana Tanzania nzima.

“Jezi yetu mpya ambayo tumeizindua kwa sasa inapatikana kila sehemu kwa wale wa Dodoma wasiwe na mashaka uzi wetu tayari umefika kila sehemu Watanzania wote mahali ambapo yapo maduka ya GSM.

“Bei rasmi ya jezi ni Shilingi 35,000,kuna utaratibu ambao upo kwa kupitia matawi na hiyo itafanya tuweze kufanikiwa malengo yetu,” .

Mbunifu wa uzi huo mpya ni Sheria Ngowi ameeleza kuwa kuna nembo za kila mahali ambazo zinaiwakilisha Tanzania kwenye uzi huo ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro,Ngome Kongwe.


VIDEO:Fahamu dhana ya Jezi yetu ya Nyumbani kwa msimu wa 2022/2023.

Hadithi yetu ya jezi ya nyumbani imeanzia kwenye kutangaza maeneo yote muhimu na ya kihistoria kwenye nchi yetu kama Mlima Kilimanjaro, Nyerere Square Dodoma, Ngome Kongwe Zanzibar, Askari Monument Dar es Salaam, Jiwe la Bismarck Mwanza na kadhalika.


VIDEO:Fahamu dhana ya Jezi yetu ya Ugenini kwa msimu wa 2022/2023.

Hadithi yetu ya jezi ya ugenini inaelezea muunganiko wa Matawi ya Wanachama Tanzania nzima ikichagizwa na mfumo wa mabadiliko.

𝗣𝗔𝗠𝗢𝗝𝗔 𝗧𝗨𝗠𝗘𝗨𝗡𝗚𝗔𝗡𝗔🔰

VIDEO:Fahamu dhana ya Jezi yetu ya Tatu (third kit) kwa msimu wa 2022/2023.

Hadithi yetu ya jezi ya Tatu (third kit) inawahusisha Wachezaji wetu wa zamani (legends) kwa kufanya makubwa katika sehemu ya historia ya Klabu yetu na jezi hii imebuniwa kwa kuwaandika majina yao kwa mfumo wa sahihi (signature)

Post a Comment

0 Comments