Ticker

6/recent/ticker-posts

Dickson Job: Sina presha na Usajili Mpya

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

BEKI kitasa wa Yanga, Dickson Job amesema licha ya usajili mkubwa uliofanywa na timu hiyo hana wasiwasi kuhusu namba yake katika kikosi cha kwanza.

Job msimu uliopita alikuwa mhimili wa Yanga katika eneo la ulinzi akicheza sambamba na nahodha Bakari Mwamanyeto, Yanick Bangala na wakati mwingine Ibrahim Bacca jambo linalomfanya kuendelea kuamini atafanya vizuri zaidi msimu ujao.


“Sina shida na usajili unaofanyika, ni mzuri na utasaidia kuimarisha timu katika msimu ujao.

“Mimi ninaamini katika ubora na kujituma hivyo sina wasiwasi kuhusu nafasi yangu ya kucheza kwani kocha ndiye ataamua ampange nani,” alisema Job.

Ujio wa kiungo Mrundi, Gael Bigirimana huenda ukamfanya kiraka Yanick Bangala kurudi nyuma eneo la ulinzi hivyo ushindani utaongezeka kwa Job, Mwamnyeto, Bacca na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aliyeongezewa mkataba wa mwaka mmoja.

Job alijiunga Yanga kwenye dirisha dogo la usajili la msimu wa 2020/21 akitokea Mtibwa alikoanzia soka timu za vijana na akatamba katika timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys.

Post a Comment

0 Comments