Ticker

6/recent/ticker-posts

Christian Eriksen: Erik Ten Hag alikuwa na mchango mkubwa mimi kujiunga Man Utd

Christian Eriksen amekiri kwamba meneja Erik ten Hag amechangia kwa kiasi kikubwa uamuzi wa yeye kujiunga na Manchester United - kitu ambacho hakukitarajia kama kingetokea, licha ya kuhusishwa mara kadhaa kujiunga na United katika maisha yake ya soka.

Eriksen amekamilisha usajili wake kujiunga United mapema hii leo kwa uhamisho huru, baada ya kumaliza mkataba wake wa muda mfupi Brentford.


Raia huyo wa Denmark alijiunga na The Bees hadi mwishoni mwa msimu baada ya mkataba wake na Inter kusitishwa. Hii ilitokana na kuwekewa kifaa maarumu kwa ajili ya mapigo ya moyo kilichowekwa baada ya kupata mshtuko wa moyo alipokuwa akiichezea Denmark kwenye Euro 2020 msimu uliopita. Kutokana na hali hiyo ilikuwa ngumu kwa Eriksen kushiriki tena katika mechi za Serie A, kulingana na sheria za nchini Italy.

Eriksen aliisaidia Brentford kusalia Ligi kuu, akifunga bao moja na kusaidia pasi za mabao manne, na timu hiyo ilikuwa bado na nia ya kutaka kuongezea muda. Hata hivyo, United walishinda swala hili na kufanikiwa kuipata saini ya Eriksen, huku Mdenmark huyo akiweka wazi kufurahishwa kwake kuwasili Old Trafford katika mahojiano yaliyotumwa kwenye tovuti ya klabu hiyo.

"Inashangaza, sikuwahi kufikiria kwamba ingetokea, kwa mimi kuwa hapa, kama unavyosema kuwa mchezaji wa Manchester United, ni kitu cha kipekee sana," Eriksen alisema. .

"Nilikuwa nikifikiria wakati wangu wa kujiunga Manchester United ulisha pita! Ni wazi, wakati huo nilikuwa Spurs, kisha nikaenda Italia, lakini sasa kuketi hapa hakika ni kitu ambacho sikutarajia, lakini pia nina furaha sana. kwamba niko hapa. Ninajisikia vizuri, ninajisikia vizuri kuwa hapa. Alisisitiza"

Eriksen aliendelea na kusema kuwa meneja Erik Ten Hag alikuwa na mchango mkubwa katika kumshawishi kuhamia Man Utd msimu huu wa majira ya joto.

"Sana. Namekuja hapa kucheza mpira, sijaja hapa kwa ajili ya nembo pekee, nimekuja hapa kucheza," alisema.

"Ni wazi baada ya kuzungumza na meneja na kusikia mawazo yake na kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala ya soka ilikuwa ni swala zuri na bora kwangu kupata uamuzi na uwezekano wa kujiunga Manchester United."

Post a Comment

0 Comments