Ticker

6/recent/ticker-posts

Ceasar Manzoki kutua Simba muda wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Ceasar Manzoki kutua SimbaSTRAIKA Mkongomani "Ceasar Manzoki" yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Simba, Manzoki ameaga rasmi wachezaji na mashabiki wa Vipers ya Uganda.

Simba imefanya mazungumzo na staa huyo wa DR Congo na wameshakubaliana ambapo mkataba wake na Klabu yake ya Vipers unamalizika Alhamisi ya wiki hii.

Msimu huu kwenye Ligi ya Uganda Mkongomani huyo ametwaa tuzo ya ufungaji bora akiwa na mabao 18, staa wa msimu na mchezaji bora wa wachezaji. 

Katika ukurasa wake jana aliandika ujumbe wa kuaga akishukuru na kusema hataisahau klabu hiyo.

Mmoja wa viongozi wa Simba alidokeza kwamba mchezaji huyo ndiye mbadala wa Meddie Kagere ambaye watatemana nae. 

Alisema kwamba Kagere amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Simba lakini lazima wafanye mabadiliko magumu ili kuirejesha Simba kwenye hadhi yake ndani na nje ya Tanzania.

Tayari Simba imeshamtambulisha, Moses Phiri kutoka zambia na habari za uhakika ni kwamba anayefuatia ni Manzoki ambaye muda wowote atakanyaga kwenye ardhi ya Tanzania. 

Winga Mkenya, Harrison Mwenda wameshindwa kuafikiana na amerudi kwao wakati akisikilizia simu ya Azam.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments