Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA YAACHANA NA ROBERTINHO

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula imesema Klabu hiyo imefikia pia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

“Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wa ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya, katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola na tayari mchakato wa kutafuta Makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde”

Robertinho ameipokea Simba kutoka kwa Juma Mgunda katikati ya msimu wakati timu ikielekea makundi ya CAFCL, kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuipeleka timu Robo Fainali kwenye kundi lenye klabu kama [Raja, Vipers na Horoya] Tinho akatoboa.

Kazi ya pili ikawa ni kuivusha Simba kwenda Nusu Fainali ambayo ni nchi ya ahadi kwao, mechi dhidi ya Wydad Casablanca Mnyama akafa kwa makuta Mohammed V Morocco [halikupita panga chini ya kivuli cha kufa kiume]

Juhudi zikabaki kwenye Ligi na ASFC kote huko mnyama akatoka patupu bila chochote [halikupita panga kwa kuwa hajaenda na timu pre-season lakini pia % kubwa ya kikosi hajasajili yeye timu ameikuta]

Ligi ikaisha mwamba akaandaa ripoti ya nani na nani anamtaka kikosini, kuhusu kuletewa anaowataka ni Klabu na kocha ndio wanajua lakini timu ilisajili akapewa pre-season nje ya nchi.

Msimu ukaanza ingia toka akaipa Simba Ngao ya Jamii bila kufunga goli wala kuruhusu goli, Preliminary round CAFCL dhidi ya Power Dynamos mnyama akatoboa roho mkononi kwa aggregate. Tinho katoboa!

Super League dhidi ya Al Ahly Simba ikawa timu ya kwanza kuaga ndani ya siku sita tangu kuanza kwa mashindano [aggregate ya 3-3], Tinho akatoboa tena!

Mara hii ikadondokea derby dhidi ya mtani, furaha ya Simba ya miaka zaidi ya 11 ni bao 5 za mwaka 2012 ikageuka kilio ndani ya dakika 30 za mwisho!

Zikaanza fununu na mwisho wa siku Taarifa kwa umma imetoka mwamba Tinho hatunaye tena Msimbazi!

Unamkumbuka kwa lipi Tinho_____?

Post a Comment

0 Comments