Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema leo ni siku ya furaha sana katika kazi yake ya ukocha, tumepata ushindi dhidi ya tibu bora [Simba]. Wachezaji wangu wamecheza vizuri sana kwa bidii, kujituma na nidhamu, naamini mashabiki wetu wamefurahi.
Tulitangulia kufunga goli kipindi cha kwanza lakini tulishindwa kulilinda, wakati wa mapumziko niongea na wachezaji ni lazima tucheze vizuri kwa namna ambavyo tumepanga kucheza. Tutulie na mpira, tumiliki mpira na tucheze kwa style yetu.
Gamondi awapa mechi nne mastaa yanga
JUMAPILI ya Novemba 5, 2023 kamwe haiwezi kusahaulika miongoni mwa wanachama na mashabiki wa Simba baada ya timu yao kufungwa mabao 5-0 na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo rekodi hii haifiki ile ya mwaka 1977 iliyowekwa na Simba ilipoifunga Yanga mabao 6-0 katika mchezo wa ligi.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Yanga yamefungwa na kenned Musonda, Max Nzengeli(mawili), Stephen Azizi Ki na Pacome.
0 Comments