Ticker

6/recent/ticker-posts

Gamondi awapa mechi nne mastaa yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha Miguel Gamondi amewataka mastaa wote waliopo kikosi cha Yanga kuonyesha uwezo wao kwenye mechi zao zijazo ili kuendelea kupata namba katika kikosi hicho.

Kikosi cha Yanga kinajifua kwa mazoezi makali ajili ya pambano la Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC litakalopigwa Oktoba 25, huku kocha wa timu hiyo, Manuel Gamondi amedaiwa kuwapa mechi nne mastaa wasiopungua watano akiwamo straika Hafiz Konkoni kabla ya kufanya maamuzi magumu.

Mastaa ambao hawajapata namba kwenye mechi za hivi karibuni ni pamoja na Crispin Ngushi ambaye alijiunga na Yanga akitokea Mbeya Kwanza, Hafiz Konkon hajawa na uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza, Aboutwalib Mshery, Gift Fred na Dennis Nkane.

Robertinho afanya kikao kizito na Wachezaji Simba Sc

Nkane amekuwa na zali lakuanzia benchi na kupata nafasi ya kucheza kwenye mechi za ligi licha ya kushindwa kuonyesha makeke yake uwanjani.

Taarifa zimeeleza kuwa mastaa hao wanapaswa kuongeza nguvu sehemu ya mazoezi na wakipata nafasi wanapaswa kufanya kweli.

Mechi tano za ligi zijazo ambazo huenda Gamondi atakuwa akifanya mabadiliko ya wachezaji kwa kumpa kila mmoja nafasi ili kuwapima wachezaji hao waliwatega ni ile ya Azam itakayopigwa Oktoba 25, kisha, Singida Big Stars, Simba, Coastal Union mbali na mechi za Ligi ya Mabingwa zinazoanza Novemba 25.

Post a Comment

0 Comments