Ticker

6/recent/ticker-posts

Young Africans yapongezwa usajili wa Maxi Zengeli

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha wa AS Vita ya DR Congo, Roul Shungu amesifu usajili mpya wa Kiungo Mshambuliaji mpya wa Young Africans, Maxi Zengeli akisema  kuwa timu hiyo, imelamba dume kwa kumsajili wa nyota huyo.

Maxi amesajiliwa na Young Africans akitokea Meniema FC ya DR Congo aliyokuwa anaichezea kabla ya kusajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili ya kukipiga hapo katika msimu ujao.

Akizungumza kabla ya safari ya kurejea DR Congo Kocha Shungu amesema kuwa, kiungo huyo bado hajaonyesha kiwango kile ambacho yeye anakifahamu, hivyo Wanayanga wajiandae kupata burudani na mafanikio kutoka kwa nyota huyo.

Ali Kamwe: Tunakwenda Tanga kuchukuwa Ngao ya Jamii

Shungu aliongeza kuwa kiungo huyo ni mchezaji hatari na wa kuchungwa hasa kwa timu pinzani ambao wana kibarua kigumu katika msimu ujao, akiamini ataipa mafanikio Young Africans.

“Niwaambie mashabiki wa Young Africans kuwa kwa sasa wanapaswa kuwa wavumilivu kwa Max, kwani hapo wanapomuona hayupo kwenye kiwango chake kile ambacho ninachokijua.

“Hiyo ni baada ya Ligi Kuu ya Congo kusimama kwa muda, hivyo amekosa mechi fitinesi na kikubwa mashabiki hao wampe muda ninaamini hawatajutia ubora wake. “Kwani Max napokuwa kwenye ubora wake ninaojua ni mchezaji hatari sana, niwapongcze Young Africans kwa kufanikiwa usajili huo ambao mimi nauunga mkono, ni usajili bora ambao wameufanya,” amesema Shungu.

Post a Comment

0 Comments