Ticker

6/recent/ticker-posts

Gamondi afurahishwa na Makipa Young Africans

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans,Kutoka Argentina Miguel Gamondi anatajwa kuwa kwenye furaha kuwaona Walinda Lango watatu wakiwa kwenye uimara mazoezini.

Young Africans ambayo ina kazi ya kutetea mataji yake msimu huu 2023/24, kwenye upande wa Walinda Lango wapo watatu wakiongozwa na Djigui Diarra raia wa Mali.

Djigui ana tuzo ya kipa bora na yupo kwenye orodha ya kikosi bora msimu wa 2022/23 wengine ni Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery ambao hawa ni wazawa.

Taarifa kutoka Young Africans zimeeleza kuwa makipa wote wanampa furaha Gamondi kambini kutokana na kuwa makini kutimiza majukumu yao.

Robertinho awatuliza Mashabiki Simba SC

“Kocha anafurahia uwepo wa makipa mazoezini kwa namna wanavyotimiza majukumu yao anaamini kuwa wote wakiwa imara ni mwendelezo wa kuchagua nani ataanza kwenye kikosi cha kwanza,” ilieleza taarifa hiyo.

“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kutimiza majukumu hivyo tuna amini kwamba tutafanya vizuri kwenye mashindano tunayoshiriki.” Amesema Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe

Post a Comment

0 Comments