Ticker

6/recent/ticker-posts

Viongozi Simba Sc Wanapambana kumbakiza Chama

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kiungo wa Simba SC Clatous Chota Chama ameshindwa kuondoka jijini Dar es salaam leo Jumatatu (Julai 17) kuelekea nchini Uturuki kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao.

Chama alitakiwa kuondoka sambamba na wachezaji wenzake Jean Baleke, Willy Onana na Che Malone lakini imeshindikana kufuatia ishu yake, kwani kesho ana kikao kingine na mabosi wa Simba SC.

Simba SC kutambulisha Wengine watatu

Chama amezua taharuki baada ya kutaka kuboreshewa masilahi yake kama makubaliano waliyoingia na uongozi aliporejea kutoka RS Berkane ya Morocco akipewa mkataba wa miaka miwili na nusu kabla ya kupunguzwa kutokana na kiwango na majeraha aliyokuwa nayo, alikutana viongozi Ijumaa (Julai 14), lakini muafaka haujapatikana.

“Chama atakutana na viongozi Jumanne (Julai 18) kuendelea kujadili ishu yake, hivyo ni ngumu kuondoka na wenzake, huenda atasafiri Alhamisi akiwa na wachezaji wengine akiwamo Luis kwenda kuongeza nguvu kambini,” kimesema chanzo hicho na kuongeza;

“Jean Baleke, Willy Onana na Che Malone hawa ndio nina uhakika wameondoka leo Jumatatu, lakini kwa Chama nadhani ni baada ya kikao na viongozi wa Simba SC kinachofanyika kesho Jumanne.”

Kouassi Atohoula mrithi wa Djuma Shaban Yanga

Viongozi wa Simba SC wamekuwa wakitafutwa kwa njia ya simu, lakini simu zao zinata bila kupokelewa na hata wakitumiwa ujumbe ili kutoa ifafanuzi wa baadhi ya mambo hayo hawakuwa tayari kujibu.

Post a Comment

0 Comments