Ticker

6/recent/ticker-posts

Usajili wa Luis Miquissone Simba SC wazua gumzo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Usajili wa Kiungo Luis Miquissone aliyerejeshwa Simba Sc akitokea Al Ahly ya Misri umegeuka gumzo kila kona kutokana na kukonga nyoyo za wanasimba na baadhi ya wadau wa soka ndani na nje ya nchi.

Usajili huo umeonekana kama muarubaini kwa timu hiyo iluiyopoteza mataji yote iliyokuwa nayo kwa misimu miwili mfululizo mbele ya Young Africans na kufanya wadau kumjadili tangu alipotambulishwa juzi Jumamosi (Julai 22) mchana.

Chama aupongeza uongozi wa Simba SC kwa Usajili

Mmoja wa wanachama wa Simba wanaoishi Afrika Kusini, Abdullah Mabange amesema kuwa, kurejea kwa fundi huyo ni moja ya sajili zilizokuwa zikililiwa kwa muda mrefu na wanasimba na kwamba kilichobaki ni kuona mziki wa Msimbazi ukiwafunika wapinzani.

“Nawapongeza sana viongozi wa klabu yetu kwa kutupa amani ya moyo, huyu fundi bwana karudi atakutana na mafundi wenzake maana ujio wake kuna watu hawakulala,” amesema Mabange aliyeongeza hata nyota wengine waliosajiliwa na kubakizwa kikosini ni wazuri na ndio maana wamesajiliwa kuitumikia time ya yenye mafanikio makubwa ndani na nje.

Kwa upande wa kocha na mchambuzi wa soka, Kennedy Mwaisabula amesema usajili wa Luis umekuja wakati muafaka ambao Simba inapambana kurejesha furaha kwa mashabiki wao.

Habari Kubwa Za Magazeti Ya Leo July 25, 2023

“Miquissone( Luis) ni mchezaji ambaye upenda wa pili hawataki wala hawahitaji kumsikia, ni usajili mzuri na mkubwa sana nawapongeza Simba katika kutimiza kiu ya wapenzi wa klabu yao,” amesema Mwaisabula.

Kocha huyo amesema wale wanaohoji alifanya nini alipokuwa Al Ahly au Abha wanapaswa kutulia kwani anaamini atafanya vizuri hapa kutokana na mahitaji yake na ubora aliokuwa nao.

Luis ataungana na nyota wapya waliotimba kambini juzi akiwamo kipa Jefferson Luis kutoka Brazili aliyetambulishwa jana Jumapili (Julai 23) kama tulivyowahabarisha, Chilunda, Kazi na Hamis.

Pia kuna wachezaji wapya kama Fabrice Ngoma, Aubin Kramo, Willy Onana, David Kameta ‘Duchu’ na beki Mcameroon, Che Fondoh Malone, waliochukua nafasi ya nyota 10 waliotemwa katika kikosi kilichopita kilichomaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara.

Post a Comment

0 Comments