Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais Yanga:Awatoa hofu mashabiki.....Tulishamaliza zamani saana

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Rais wa Yanga SC Eng.Hersi Ally Saidi amewatoa hofu wapenzi wa klabu hiyo kuwa uongozi wao uko imara na utahakikisha unafanya kila linalowezekana ili Klabu hiyo ipate mafanikio makubwa zaidi sambamba na kukusanya mataji kwa kadri inavyowezekana ili kuendeleza furaha Jangwani.

Eng.Hersi amesema hayo leo, Julai 10.2023 alipokuwa akizungumza mara baada ya timu hiyo kupokea mfano wa Hundi ya shilingi milioni 405 kutoka kwa wadhamini wao wakuu, kampuni ya ubashiri wa michezo ya Sport Pesa, kwenye hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, fedha ambayo ni Bonasi baada ya Timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali iliyoshiriki msimu uliopita ikiwemo mchezo wa ngao ya jamii, Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBCPL), Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambazo yote walitwaa makombe yake, sambamba na kucheza fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika

Ally Kamwe amtaja Namba 06 wa Young Africans

"Ninatimiza mwaka mmoja toka nilipopata nafasi ya kuwa Rais wa Klabu ya Young Africans, imani yenu kwangu imeendelea kutufanya kuwa imara na kufanikiwa katika msimu huu uliopita, na naomba nipate imani hiyo kwenu katika kipindi cha miaka mitatu iliyobaki, tukianza na msimu huu wa pili katika uongozi wangu..."

"Kuiamini administration hii ambayo nyie kwa nafasi ya kikatiba mlitupatia tukaisimamia Klabu hii kwenda kwenye mafanikio...., haya yanayoendelea sijuwi nani kasajili, nani kafanya hivi, sisi tushafanya hayo muda mrefu saana na timu yetu iko imara saana, na tutakuwa imara zaidi ya ilivyokuwa mwaka jana, tutakuwa hapa kwaajili ya kutangaza mafanikio tena, na nafikiri mwakani utaifanya kama tarehe hii ya leo Mungu akipenda, tukiwa tunakabidhiwa hundi kama hizi za mafanikio...".

Che Fondoh Malone atambulishwa Simba Sc

Post a Comment

0 Comments