Ticker

6/recent/ticker-posts

Kylian Mbappe Apewa Wiki Mbili PSG Kuongeza Mkataba au Kuondoka

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KLABU ya PSG  ya nchini ufaransa imempa Mshambuliaji Kylian Mbappe muda wa wiki mbili kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake kuhusu kuongeza mkataba Mpya.

Mbappe alithibitisha mwezi uliopita kwamba hatasaini mkataba mpya na PSG haipo tayari kumpoteza Mbappe bila malipo na wanataka yeye afanye uamuzi haraka la sivyo Aondoke.

Rais wa klabu ya Paris Saint-Germain Nasser Al-Khelaifi ameeleza wazi msimamo wa klabu hiyo kuhusu mzozo wa uhamisho unaomhusisha Kylian Mbappe.

Granit Xhaka atimka Arsenal baada ya miaka 7

PSG imekumbwa na mgogoro na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye anataka kuondoka bure msimu ujao. 

Mkataba wa sasa wa Mbappe na Les Parisiens una kifungu cha kuongeza mwaka mmoja ambapo anaweza kutumia kifungu hicho kuongeza mkataba, lakini mchezaji huyo amekata. 

PSG haina chaguo lingine zaidi ya kumuuza katika dirisha hili la uhamisho ili kuepuka kumpoteza bure wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu ujao, kulingana na ripoti kutoka jarida la Reuters.  

Wakati wa uzinduzi wa kocha mpya Luis Enrique siku ya Jumatano, Rais wa Paris Saint-Germain Nasser Al-Khelaifi alitoa muda wa mwisho kwa Mbappe wakati mzozo wa mkataba unaendelea. 

Man United kukamilisha Usajili wa Kipa Andre Onana kutoka Inter Milan muda wowote

"Kylian Mbappe... lazima afanye uamuzi wiki ijayo au wiki mbili zijazo. Sio zaidi ya hapo. Ikiwa hataki kusaini mkataba mpya, mlango uko wazi," alisema rais huyo kwa ukali. Akisisitiza umuhimu wa hali inayohusisha Mbappe, Al-Khelaifi alibainisha kwamba hakuna mchezaji anayeshikilia umuhimu mkubwa kuliko klabu yenyewe.

"Hakuna mtu anayekuwa mkubwa kuliko klabu, hakuna mchezaji, hata mimi. Ni wazi sana," alisema kwa mujibu wa Le Parisien, kama alivyonukuliwa na mtaalamu wa uhamisho, Fabrizio Romano

Post a Comment

0 Comments