Ticker

6/recent/ticker-posts

Kouassi Atohoula mrithi wa Djuma Shaban Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Uongozi wa Klabu ya Yanga unatarajia kumpokea beki wa kulia wa ASEC Mimosas ya vory Coast, Kouassi Atohoula, kwa ajilĂ­ ya kukamilisha shughuli ya Kusaini mkataba, kisha kutambulishwa rasmi kama mrithi wa Djuma Shaban.

Taarifa za kina kuwa, tayari nyota huyo ameshakamilisha kila kitu kwa ajili ya kutua klabuni hapo, na alitarajiwa kutua muda wowote kuanzia sasa.

Yanga yamuwinda Kouassi Attohoula kutoka ASEC Mimosas

Tunamshukuru Mungu baada ya Djuma Shaban kuonesha hali ya kugomea mkataba mpya na kupishana kauli kwenye mambo kadhaa na uongozi, mara moja tuaanza taratibu za kutafuta mbadala wake ambapo tayari tumekamilisha usajii wa beki wa kulia kutoka ASEC Mimosas ya lvory Coast, Kouassi Attohoula na atatua nchini juma hili tayari kwa kuinga kambini na wenzake, mmoja wa viongozi amedokeza wakati akihojiwa.

Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema: “Wachezaji wote wataanza kuingia nchini kwa ajii ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao, wataungana na wachezaji wapya wote ambao usajili wao umekamilika, kisha tutaanza kutangaza mmoja baada ya mwingine.”

Post a Comment

0 Comments