Ticker

6/recent/ticker-posts

Granit Xhaka atimka Arsenal baada ya miaka 7

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya soka ya Arsenal imethibitisha kumuuza nahodha wake msaidizi Granit Xhaka kwa Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa kitita cha pauni milioni 21.4.

Arsenal ilithibitisha katika taarifa yake siku ya Alhamisi jioni kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 amejiunga na klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

"Granit Xhaka amejiunga na klabu ya Bundesliga ya Bayer Leverkusen kwa uhamisho wa kudumu," klabu ya Arsenal ilitangaza kupitia tovuti yake.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uswisi anaondoka katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuichezea kwa takriban miaka saba tangu ajiunge nayo mwezi Mei 2016. Alihusika katika jumla ya mechi 297 ambapo alifunga mabao 23.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alimsifu kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 wakati akiiaga klabu hiyo na kumtakia heri katika safari yake mpya.

Mason Mount awaaga mashabiki wa Chelsea kabla ya kujiunga na Manchester United

“Granit amekuwa sehemu kubwa ya klabu yetu kwa muda mrefu. Amejitolea na ubora kwa miaka mingi, akicheza jukumu muhimu katika maendeleo na mafanikio yetu. Anatuacha na heshima na shukrani zetu kubwa. Tunamtakia Granit kila la kheri kwa siku zijazo,” Arteta alisema.

Bayer Leverkusen pia ilithibitisha kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi kupitia mitandao yake rasmi.

"Granit Xhaka amesaini mkataba hadi 2028 kwenye uwanja wa Bay Arena," Leverkusen ilitangaza siku ya Alhamisi jioni.

Katika klabu hiyo ya Ujerumani, Xhaka atavaa jezi namba 34 ambayo alikuwa akiivaa akiwa Arsenal.

Post a Comment

0 Comments