Ticker

6/recent/ticker-posts

Fabrice Luamba Ngoma kutua Simba SC ni suala la muda tu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mazungumzo kati ya uongozi wa Klabu ya Simba na Klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan inayo mmiliki kiungo Fabrice Luamba Ngoma yanaenda vizuri na muda wowote kiungo huyo Ata tambulishwa Msimbazi.

Ngoma anaripotiwa kuvunja mkataba wake na klabu yake ya Al Hilal Omdurman ya Sudan kutokana na ligi kusimama kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo, lakini hata hivyo klabu hiyo imemjia juu kiungo huyo ikidai hajafuata taratibu zinazotakiwa, hivyo Simba SC wapo kwenye mazungumzo na Al Hilal Omdurman ili wamsajili kiungo huyo.

Che Fondoh Malone atambulishwa Simba Sc

Taarifa za kina kutoka Simba SC zinaeleza kuwa: “Simba SC imekamilisha taratibu zote za usajili wao hivyo kilichobaki kwa sasa ni utambulisho wa wachezaji ambao bado hawajatambulishwa.

“Ukiangalia mipango ya uongozi ni kuhakikisha kuwa wanamtambulisha Fabrice Ngoma mwishoni na ndio maana utaona tayari kuna wachezaji wametambulishwa mapema lakini Ngoma bado hajatambulishwa.

“Hiyo ni mipango ambayo wanaona kuwa Ngoma akitambulishwa mwishoni litakuwa jambo kubwa kwa kuwa ni usajili ambao uliimbwa sana kutokana na klabu hiyo kuhusiswa na kuwapokonya Young Africans mchezaji huyo,” kimeeleza chanzo hicho

Yanga Yamalizana na Gift Fred

Kwa upandea Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally yeye amesema: “Simba SC msimu huu kila usajili ni usajili mkubwa na hakuna sijui usajili huu wa kawaida wala ule mkubwa kuliko huu, kila usajili utakuwa tishio jambo ambalo wanasimba wanatakiwa kulifanya ni kuendelea kuwa karibu na sisi kwani tutashusha vyuma vya maana.

Post a Comment

0 Comments