Ticker

6/recent/ticker-posts

Fabrice Luamba Ngoma atambulishwa Simba SC rasmi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Simba leo imemtambulisha kiungo Fabrice Luamba Ngoma kama mmoja wa wachezaji wake wapya kuelekea msimu mpya wa 2023/24.

Ngoma anaripotiwa kuvunja mkataba wake na klabu yake ya Al Hilal Omdurman ya Sudan kutokana na ligi kusimama kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo, lakini hata hivyo klabu hiyo imemjia juu kiungo huyo ikidai hajafuata taratibu zinazotakiwa, hivyo Simba SC wapo kwenye mazungumzo na Al Hilal Omdurman ili wamsajili kiungo huyo.

Simba SC kutambulisha Wengine watatu

“Simba SC imekamilisha taratibu zote za kumsajili Ngoma baada ya mazungumzo na klabu yake ya Al Hilal Omdurman ya Sudan kwenda vizuri .

Kwa upandea Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally yeye amesema: “Simba SC msimu huu kila usajili ni usajili mkubwa na hakuna sijui usajili huu wa kawaida wala ule mkubwa kuliko huu, kila usajili utakuwa tishio jambo ambalo wanasimba wanatakiwa kulifanya ni kuendelea kuwa karibu na sisi kwani tutashusha vyuma vya maana.


Post a Comment

0 Comments