Ticker

6/recent/ticker-posts

Che Fondoh Malone atambulishwa Simba Sc

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

𝐎𝐅𝐅𝐈𝐂𝐈𝐀𝐋: Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kumsajili mlinzi wa kati Che Fondoh Malone Jr almaarufu ‘Ukuta wa Jericho’ kwa ada ya uhamisho inayotajwa kuwa dola 100,000 (Tsh milioni 243) kutoka klabu ya CottonSports ya Cameroon.

Che Malone (24) raia wa Cameroon amesaini mkataba wa miaka miwili mpaka Juni 2025 na anatua klabuni hapo kama mbadala wa Joash Onyango (30) aliyetimkia Singida Fontaine Gate FC.

Leandre Onana atambulishwa Simba SC rasmi

Che Malone ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Ligi Kuu ya Cameroon msimu uliopita wa 2022/23 (2022/23 Cameroon Elite One Footballer of the Year) kwenye tuzo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Jumamosi (Julai 08) na Mboa Foot Awards huko Cameroon.

Che Malone Jr almaarufu ‘Ukuta wa Yericko’ (Wall Of Jericho) Msimu uliopita aliiongoza Cotton Sports kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Cameroon huku akicheza takribani mechi zote kama Nahodha wa klabu hiyo.

Aubin Kramo wa Asec Mimosas atua Simba Sc

Post a Comment

0 Comments