Ticker

6/recent/ticker-posts

Cedric Kaze kuwa kocha mkuu Namungo FC

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze yupo katika hatua za mwisho kujiunga na Klabu ya Namungo FC kama kocha mkuu wa benchi la ufundi la timu hiyo ya Ruangwa mkoni Lindi.

Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa Kaze yuko kwenye mazungumzo na uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi ambalo kwa sasa liko chini ya kocha Denis Kitambi.

“Kaze anakuja kuwa kocha mkuu na Kitambi atakuwa msaidizi huku Nsajigwa (Shadrack) akiendelea na majukumu yake ya kocha wa viungo,” kilieleza chanzo chetu makini ndani ya klabu hiyo.

Miguel Angel Gamondi Afurahishwa na kiwango cha Wachezaji wa Yanga

Katibu Mkuu wa Namungo FC, Ally Suleimani, alipo tafutwa ili kujua ukweli nae alisema watafanya maboresho kwa kuongeza nguvu katika benchi lao la ufundi na suala hilo linafanyiwa kazi na kamati ya mashindano kulingana na mahitaji ya timu hiyo.

“Timu yetu ipo Karatu chini ya kocha wetu Kitambi akisaidiana na Nsajigwa, ninaimani kutakuwa na maboresho ambayo yanafanywa na kamati husika,” alisema Katibu huyo.

Kuhusu Kaze, alisema ni mapema  kulizungumzia suala la kocha huyo kwa sababu liko kwenye kamati ya mashindano wanalifanyia kazi ikiwamo suala zima la maboresho ya timu yao katika kila sekta.

Kikosi cha Namungo FC kimeweka kambi Karatu, Arusha na kitacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Singida Fountain Gate FC, mchezo utakaopigwa leo, mkoani humo.

Kikiwa huko kitacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kurejea Dar es Salaam na kucheza mingine miwili na baada ya hapo kitarudi maskani kwao, Ruangwa, Lindi tayari kwa kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 15, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments