Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa
Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema hatima ya aliyekuwa Kocha msaidizi klabuni hapo Cedric Kaze, itafahamika mara baada ya kupatikana kwa Kocha Mkuu, huku pia ukiweka wazi kila kitu kuhusu Yannick Bangala na Tuisila Kisinda ndani ya kikosi hicho.
Afisa Habari wa Klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kumpata Kocha Mkuu na atakapokabidhiwa majukumu ndiye atakayeamua kuendelea kufanya kazi na benchi lililopo akiwamo Kaze, au kuja na watu wake.
Kutokana na hali hiyo, hatima ya Kocha huyo raia wa Burundi kubaki Yanga au kuondoka, itategemea maamuzi ya Kocha Mkuu atakayekuja.
Lomalisa Aomba Kuvunja Mkataba Yanga
“Sasa hivi mazungumzo yaliyopo ni kumpata Kocha Mkuu, tukishampaka ndiyo tunampa fursa ya kuchagua wasaidizi wake, akitoa ruhusa tutaendelea na mazungumzo, yeye ndiye atakayetuambia watu gani anaotaka kufanya nao kazi kwenye Benchi lake la Ufundi.
“Akisema anawahitaji sawa, lakini anaweza kusema anakuja na Benchi lake la Ufundi, ndiyo dunia ya mpira wa sasa ilipofikia na sisi Yanga ni weledi,” amesema Kamwe
Kuhusu Yannick Bangala na Tuisila Kisinda
Akizungumzia juu ya taarifa za mchezaji wao Bangala kutaka kuondoka, amesema kwa sasa ni mchezaji wa Yanga aliyebakisha mwaka mmoja lakini kama akipata ofa nono, yenye maslahi kwa pande zote mbili klabu haiwezi kumzuia.
“Mpaka sasa ana mkataba wa mwaka mmoja, na mwaka wake uliobakia tunapitia ripoti ya Benchi la Ufundi tukisubiri kumpata Kocha Mkuu mpya, lakini tunaongea na mchezaji mwenyewe, halafu hatima yake itatolewa,” amesema
Kuhusu kuachana na Tuisila Kisinda, Kamwe amesema amemaliza mkataba wake wa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Klabu ya RS Berkane na sasa anarejea huko.
0 Comments