Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga kumuongeza mkataba kocha Nasreddine Nabi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Uongozi wa Klabu ya Yanga chini ya Injinia Hersi Said umevunja ukimya juu ya hatma ya kocha wao Nasreddine Nabi ukisema kocha huyo bado ataendelea kubaki klabuni hapo.

Hersi ameyasema hayo wakati akihojiwa asubuhi hii na kituo cha Radio Cha Wasafi akisema Yanga bado inamuhitaji Nabi.

Gadiel Michael kurudi Azam FC

"Kila mkataba una kikomo nikweli mkataba wa Nabi unafikia tamati mwisho wa msimu huu na klabu ilishaanza hatua ya kumuongezea mkataba mwingine,"amesema Hersi.

Aidha Hersi ameongeza kuwa tayari Nabi ameshamleta nchini mwanaye Hedi Nabi ambaye ndio msimamizi wake wa masuala ya mkataba katika hatua za mwisho za kusaini mkataba mpya.

"Jana tumerejea nchini nadhani Maulid (Kitenge) ulikuwepo kwenye ndege umemuona mtoto wa Nabi (Hedi) tulirudi naye alikuja kutoka kwao akafikia Algeria akaangalia na mchezo na ujio wake ni pamoja na kusimamia hii hatua ya kusaini mkataba mpya wa kubaki Yanga.

"Niwatoe hofu Wanayanga kwamba Nabi Yuko hapa na atabaki zaidi kuendelea kukisuka kikosi chetu."

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo amefunguka kuhusu mustakabali wa Beki wa kati kutoka visiwani Zanzibar Ibrahim Bacca ambaye amekuwa kigigi mujaraab kwa timu pinzani tangu alipoanza kupewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Young Africans.

Hersi amesema Beki huyo ameshasaini mkataba mpya ambao unamuwezesha kulipwa fedha nyingi klabuni hapo, hivyo amewasisitiza Mashabiki na Wanachama kuendelea kumpa ushirikiano Bacca waliyemsajili msimu uliopita akitokea KMKM ya kwao Zanzibar.

“Hii ni Exclusive ambayo naitoa hapa. Ibrahim Bacca Tumemuongezea Mkataba na mshahara mkubwa. Siwezi kuutaja hapa kwa sababu ni mkataba wa siri wa pande mbili” amesema Hersi

Post a Comment

0 Comments