Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa
Wakala wa Mshambuliaji Ranga Chivaviro amemaliza utata kuhusu tetesi za Mshambuliaji huyo kutakiwa na mabingwa wa soka Tanzania Bara Young Africans msimu ujao 2023/24.
Kampuni ya TNB Sports Agency Management inayomsimamia Ranga Chivaviro chini ya Mkurugenzi Herve Tra Bi imesema ni kweli walikuwa na mazungumzo na Rais wa Young Africans Hersi Said, kwa ajili ya kufanya biashara ya usajili wa Chivaviro, lakini kwa sasa mpango huo umekufa kufuatia Klabu za Kaizer Chiefs na Orlando Pirates kuweka fedha nyingi, kwa ajili ya uhamisho wa Mshambuliaji huyo.
Uongozi Simba SC: Hatutakosea usajili 2023/24
Kiongozi huyo amesema wanauheshimu Uongozi wa Young Africans kupitia Rais wake Hersi Said, lakini kwa mpango wa uhamisho wa mchezaji wao hawana budi kuwataka radhi kwa kusitisha mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ili kufanikisha biashara kati yao na Kaizer Chiefs ama Orlando Pirates zote za Afrika Kusini.
“Tunamuheshimu Rais wa Young Africans, lakini kwa sasa hakuna uwezekano wa Ranga Chivaviro kutua katika klabu hiyo ya Tanzania, awali tulikuwa na mazungumzo ambayo yalikwenda vizuri sana lakini mambo yamebadilika.”
“Mchezaji alikuwa ameshakubali kucheza soka Tanzania, lakini ofa zilizowasilishwa kwetu zimebadili kila kitu na sasa kuna uwezekano wa Chivaviro kubaki Afrika Kusini.”
“Klabu za Kaizer Chiefs na Orlando Pirates zimeleta ofa bora zaidi, na sisi TNB Sports Agency Management tumeona tufanye biashara nzuri kwa maslahi ya mchezaji wetu.” Amesema Mkurugenzi Herve Tra Bi
0 Comments