Ticker

6/recent/ticker-posts

Uongozi Simba SC: Hatutakosea usajili 2023/24

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Uongozi wa Klabu ya Simba SC umeweka wazi kuwa utafanyia kazi mapendekezo ya Benchi la Ufundi kwenye upande wa usajili ili kuongeza wachezaji imara ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao.

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ambaye kwa sasa yuko mapumzikoni nchini Brazil amewaomba viongozi wa timu hiyo kuongeza wachezaji wawili wawili kila idara ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi kwa msimu ujao.

Tetesi za usajili Mpya: Simba SC Kusajili kimya kimya

Kukamilika kwa usajili ndani ya Simba SC kutamrahisishia Oliveira kwenye utendaji wake katika kupambania malengo kuanzia msimu ujao 2023/24.

Simba SC imepishana na mataji yote iliyokuwa inapambania ikiwa ni pamoja na ligi, Azam Sports Federation, Ngao ya Jamii, Kombe la Mapinduzi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika huku ikigotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 73.

Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema: “Kwa namna ambavyo tumefanya kwenye ligi hatujapenda kwani malengo yetu hayajafikiwa hivyo ambacho tunakifanya ni kufanyia kazi makosa yaliyopita na kufanya usajili mzuri kwenye kila idara.

Luis Miquissone awavuruga mabosi Simba SC

“Kikubwa ambacho tunahitaji kwa msimu ujao ni kuwa tofauti na kupata kile ambacho tunahitaji. Usajili wetu ujao tunaamini utakuwa mzuri na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa kwani tunaendelea vizuri.”

KUHUSU KUACHANA NA BAADHI YA NYOTA WAKE

Wakati huohuo, Simba SC imetangaza kuachana na wachezaji wake wa kimataifa Victor Akpan raia wa Nigeria na Mohamed Outtara raia wa Ivory Coast.

Habari Kubwa Za Magazeti Ya Leo June 22, 2023

Post a Comment

0 Comments