Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Soka barani Ulaya Jumatano 21.06.2023

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Arsenal wametoa ofa iliyoboreshwa ya £60m kwa mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Kai Havertz, 24. Kai Havertz alijiunga na Chelsea kwa £71m kutoka Bayer Leverkusen mnamo 2020 (Mail).

Fulham wanataka kumsajili kiungo wa Brazil Fred, 30, anayechezea klabu ya Manchester United. (Telegraph)

Everton wana nia ya kumnunua kipa wa Crystal Palace na Uingereza Sam Johnstone, 30, ikiwa Jordan Pickford ataondoka katika klabu hiyo. (Sun)

Leicester City wanataka zaidi ya pauni milioni 50 kumnunua kiungo wa Uingereza James Maddison, 26, huku Tottenham na Newcastle zikimwania. (Sky Sports).

Tetesi za Soka Barani Ulaya Jumamosi 10.06.2023

Manchester City wanakaribia kuafikiana kibinafsi na beki wa RB Leipzig wa Croatia Josko Gvardiol, 21. (Fabrizio Romano)

Newcastle wanafikiria kusitisha nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Inter Milan na Italia Nicolo Barella, 26. (Independent).

Crystal Palace wanamtaka Roy Hodgson mwenye umri wa miaka 75 kusalia kama mkufunzi. (Guardian)

Lakini Newcastle inapania kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Derry Scherhant, 20, kutoka Hertha Berlin. (Telegraph)

Manchester City, Chelsea na Liverpool wanawania kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Uruguay Fede Valverde, 24, msimu huu. (Teamtalk)

Post a Comment

0 Comments