Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Yatangaza Kuachana na Augustine Okrah

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Uongozi wa Klabu ya Simba sc unatangaza rasmi kuachana na kiungo wetu mshambuliaji Augustine Okrah baada ya kumalizika Msimu wa mashindano wa 2022/23.

Okrah raia wa Ghana amemaliza mkataba wake ndani ya Simba sc na mchezaji huyo hatoongezewa mkataba mpya.

Simba Yakamilisha Usajili wa Wonlo Coulibaly kutoka ASEC Mimosas

Okrah alijiunga na Simba sc mwanzoni kwa msimu huu akitokea Benchem United ya nyumbani kwao Ghana ambapo ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi zote alizocheza.

Katika msimu mmoja aliohudumu ndani ya kikosi cha Simba Okrah amekuwa na mchango mkubwa akicheza mechi 17 na kufunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa jingine moja.

Kuondoka kwa Okrah ni ishara ya kuanza rasmi utelekezaji wa maboresho ya kikosi cha Simba sc kuelekea msimu ujao wa mashindano

Uongozi wa Simba sc umedhamiria kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi kuanzia eneo la benchi la ufundi kwa kuongeza watalaamu zaidi pamoja na wachezaji wenye hadhi kubwa na ubora wa kuitumikia Simba.

Post a Comment

0 Comments